Acts 20

1Baada ya ghasia kumalizika, Paulo aliwaita wanafunzi na kuwatia moyo. Kisha kuwaaga na akaondoka kwenda Makedonia. 2Naye akiishakupita mikoa hiyo na alikuwa akiwatia moyo waamuni, akaingia Uyunani. 3Baada ya yeye kuwa pale kwa muda wa miezi mitatu, njama ziliundwa dhidi yake na Wayahudi alipokuwa akikaribia kusafiri kwa njia ya bahari kuelekea Shamu, hivyo aliazimu kurudi kupitia Makedonia.

4Walioandamana naye hadi Asia walikuwa Sopatro, mwana wa Pirho kutoka Berea; Aristariko na Sekundo, wote kutoka waamini wa Wathesalonike; Gayo wa Derbe; Timotheo; Tikiko na Trofimo kutoka Asia. 5Lakini watu hawa wamekwisha tangulia na walikuwa wanatungojea kule Troa. 6kwa njia ya Bahari kutoka Filipi baada ya siku za mikate isiyotiwa chachu, na katika siku tano tukawafikia huko Troa. Tulikaa huko kwa siku saba.

7Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekusanyika pamoja ili kuumega mkate, Paulo alizungumza na Waamini. Alikuwa akipanga kuondoka kesho yake, hivyo akaendelea kuongea hadi usiku wa manane. 8Kulikuwa na taa nyingi katika chumba cha juu ambapo tulikuwa tumekusanyika pamoja.

9Katika dirisha alikuwa amekaa kijana mmoja jina lake Utiko, ambaye alielemewa na usingizi mzito. Hata Paulo alipokuwa akihutubu kwa muda mrefu, kijana huyu, akiwa amelala, akaanguka chini kutoka ghorofa ya tatu na aliokotwa akiwa amekufa. 10Lakini Paulo alishuka chini, alijinyoosha yeye mwenyewe juu yake, akamkumbatia. Kisha akasema, “Msikate tamaa, kwa kuwa yu hai.”

11Kisha akapanda tena ghorofani na akaumega mkate, akala. Baada ya kuzungumza nao kwa muda mrefu hadi alfajiri, akaondoka. 12Wakamleta yule kijana akiwa hai wakafarijika sana.

13Sisi wenyewe tulitangulia mbele ya Paul kwa meli na tukaelekea Aso, ambapo sisi tulipanga kumchukua Paul huko. Hiki ndicho yeye mwenyewe alitaka kufanya, kwa sababu alipanga kwenda kupitia nchi kavu. 14Alipotufikia huko Aso, tukampakia kwenye Meli tukaenda Mitilene.

15Kisha sisi tukatweka kutoka huko na siku ya pili tulifika upande wa pili wa kisiwa cha Kio. Siku iliyofuata, tukawasili kisiwa cha Samo, na kesho yake tukafika mji wa Mileto. 16Kwa sababu Paulo alikuwa ameamua kusafiri kupitia Efeso, ili kwamba asitumie muda wowote katika Asia; kwa maana alikuwa na haraka ya kuwahi Yerusalemu kwa ajili ya sikukuu ya Pentekoste, kama ingeliwezekana yeye kufanya hivyo.

17Kutoka Mileto akatuma watu hadi Efeso na akawaita wazee wa Kanisa. 18Walipofika kwake, akawaambia, ninyi wenyewe mwajua tangu siku ya kwanza nilipokanyaga hapa Asia, jinsi nilivyokuwa kwenu muda wote. 19Nimemtumikia Bwana kwa unyenyekevu wote na kwa machozi, na mateso yaliyonipata mimi kwa hila za Wayahudi. 20Mwajua jinsi ambavyo sikujizuia kutangaza kwenu kitu chochote ambacho kilikuwa muhimu, na jinsi mimi nilivyowafundisha wazi wazi na pia kwenda nyumba kwa nyumba. 21Mnajua jinsi mimi nilivyoendelea kuwaonya Wayahudi na Wayunani juu ya toba kwa Mungu na imani katika Bwana wetu Yesu.

22Na sasa, angalieni, mimi, nikiwa ninamtii Roho Mtakatifu kuelekea Yerusalemu, nisiyajue mambo ambayo yatanitokea mimi huko, 23ila kwa kuwa Roho Mtakatifu hunishuhudia mimi katika kila mji na anasema kwamba minyororo na mateso ndivyo vinavyoningojea. 24Lakini mimi si kufikiria kwamba maisha yangu ni kwa njia yoyote ya thamani kwangu, ili niweze kumaliza mwendo wangu na huduma niliyopokea kutoka kwa Bwana Yesu, kuishuhudia injili ya neema ya Mungu.

25Na sasa, tazama, najua kwamba wote, miongoni mwa wale nilioenda kuwahubiri Ufalme, hamtaniona uso tena. 26Kwa hiyo nawashuhudia leo hii, kwamba sina hatia kwa damu ya mtu yeyote. 27Kwa maana sikujizuia kuwatangazia mapenzi yote ya Mungu.

28Kwa hiyo iweni waangalifu juu yenu ninyi wenyewe, na juu ya kundi lolote ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi. Iweni waangalifu kulichunga kusanyiko la Bwana, ambalo alilinunua kwa damu yake mwenyewe. 29Najua kwamba baada ya kuondoka kwangu, mbwa mwitu wakali wataingia kwenu, na wasilihurumie kundi. 30Najua kwamba hata miongoni mwenu wenyewe baadhi ya watu watakuja na kusema mambo mapotovu, ili kuwavuta wanafunzi wawafuate wao.

31Kwa hiyo muwe macho. Kumbukeni kwamba kwa miaka mitatu sikuweza kuacha kuwafundisha kila mmoja wenu kwa machozi usiku na mchana. 32Na sasa mimi nawakabidhi kwa Mungu, na kwa neno la neema yake, ambalo laweza kuwajenga na kuwapa urithi pamoja nao wote waliowekwa wakfu kwa Mungu.

33Sikutamani fedha, dhahabu, au mavazi. 34Mnajua ninyi wenyewe kwamba mikono hii imenipatia mahitaji yangu mwenyewe na mahitaji ya wale waliokuwa pamoja nami. 35Katika mambo yote niliwapa mfano wa jinsi inavyopasa kuwasaidia wanyonge kwa kufanya kazi, na jinsi mnavyopaswa kukumbuka maneno ya Bwana Yesu, maneno ambayo yeye mwenyewe alisema: “Ni heri kutoa kuliko kupokea.”

36Baada ya kusema namna hii, alipiga magoti akaomba pamoja nao. 37Wote wakalia sana na kumwangukia Paulo shingoni na kumbusu. Walihuzunika zaidi ya yote kwa sababu ya kile ambacho alikuwa amesema, kwamba kamwe hawatauona uso wake tena. Kisha wakamsindikiza merikebuni.

38

Copyright information for SwaULB